UPINZANI: HAKI KWA WAATHIRIWA KABLA YA FIDIA
Muungano wa upinzani umebuni kamati maalum itakayoangazia masuala ya waathiriwa wa maandamano watakaorodheshwa kufidiwa na jopokazi lililoteuliwa na Rais William Ruto.
Haya ni kulingana na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka akizungumza katika kaunti ya Kajiado, akiongeza kuwa muungano huo utahakikisha kwamba waathiriwa wanapata haki mwanzo kabla ya fidia.
Alikuwa ameandamana na Waziri wa zamani Fred Matiang’i, aliyewataka vijana kujisajili kwa wingi kama wapiga kura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































