WANAFUNZI HEWA WAIPUNJA SERIKALI
Zaidi ya wanafunzi hewa 50,000 wamekuwa wakinufaika na mgao wa serikali wa shilingi elfu 15, uchunguzi ukionyesha kwamba baadhi ya shule ziliongeza idadi ya wanafunzi ili kuilaghai serikali.
Haya ni kwa mujibu wa katibu mkuu katika elimu ya msingi Julius Bitok, akisema Sakata hiyo imesababisha kufujwa kwa mamilioni ya pesa.
Bitok aliyasema haya akiwa mbele ya kamati ya elimu bungeni, akiongeza kuwa uchunguzi ulioendeshwa katika shule elfu 17 kati ya elfu 32.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































