UHC NJIA PANDA KUHUSU UHAMISHO
Mustakabali wa wahudumu wa afya zaidi ya 8,000 walio chini ya mpango wa UHC kwa mara nyingine tena wameingia njia panda, kufuatia sintofahamu baina ya wizara ya afya na baraza la magavana kuhusu uhamisho wa rekodi za malipo ya wahudumu hao.
Katika kikao na wanahabari, baraza la magavana limejitenga na mpango wa kuhamishia rekodi hizo kwa serikali za kaunti, likisema tangazo la wizara ya afya linakiuka makabaliano yao ya awali.
Kulingana na tangazo hilo, wizara ya afya imesema itakamilisha uhamisho huo mwezi ujao baada ya kile ilichotaja kuwa hesabu ya wahudumu hao kwa ushirikiano na magavana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa.
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































