#Sports

VILABU VIAJIZOLEA MINOFU KATIKA KOMBE LA VILABU LA FIFA

Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA lililomalizika hivi punde lilikuja na zawadi nzuri za kifedha kwa timu zilizoshiriki, pamoja na vilabu vinne vya Kiafrika vilivyowakilisha bara la Afrika.
Vigogo wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns ndio waliopata pesa nyingi zaidi kama klabu iliyoorodheshwa zaidi barani Afrika, na kuchukua dola milioni 13.6 (takriban Ksh1.625 bilioni).
Al Ahly na Esperance zilikuwa na viambajengo sawa na hivyo kupata dola milioni 11.6 (takriban Ksh1.496 bilioni) kila moja.
Wydad AC bado ilifikia alama ya Ksh1 bilioni, huku klabu hiyo ikipata USD 9.6 bilioni (takriban Ksh1.238 bilioni).
Mwishowe, vilabu vya Kiafrika vilipata jumla ya dola milioni 46.4 (takriban Ksh6 bilioni), msaada mkubwa kwa timu, lakini ambayo inawakilisha 4.64% tu ya pesa zote.
Huku michuano hiyo ikichezwa kila baada ya miaka minne, kutakuwa na ongezeko la ushindani wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, huku miamba hiyo ya Afrika ikitazama mashindnao hayo yatakayofanyika tena mwaka 2029.
Mabingwa Chelsea kutoka England ndio walioingiza pesa nyingi zaidi, wakitwaa dola milioni 114.6 (takriban Ksh14.783 bilioni), wakifuatiwa na washindi wa pili Paris Saint-Germain, ambao walipata dola milioni 106.9 (takriban Ksh13.79 bilioni).
Vigogo wa New Zealand Auckland City FC ndio waliopata mapato ya chini zaidi kutokana na mashindano hayo wakiwa na jumla ya mapato ya dola milioni 4.6 (takriban Ksh593 milioni).

Imetayarishwa na Nelson Andati

VILABU VIAJIZOLEA MINOFU KATIKA KOMBE LA VILABU LA FIFA

TRAVERS AONDOKA BOURNEMOUTH

VILABU VIAJIZOLEA MINOFU KATIKA KOMBE LA VILABU LA FIFA

OCHOLLA AFURAHISHWA NA KIKOSI CHAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *