NIIA PANDA YA MAKURUTU 10,000
Huenda wakenya wanaolenga kusajiliwa kama makurutu wa kujiunga na idara ya polisi wakasubiri zaidi kutokana na mvutano kati ya idara ya polisi NPS na tume ya huduma za polisi NPSC.
Licha ya idara ya polisi kulenga kuwasajili makurutu 10,000, mvutano umeibuka kati yake na NPSC hasa kuhusu ni nani mweney mamlaka ya kuendesha zoezi hilo, NPS ikishikilia kuwa ni jukumu lake.
Katika kikao cha faragha mbele ya kamati ya usalama baada ya wanahabari kuondolewa, NPSC na NPS zilikosa kuelewana kuhusu zoezi hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































