MAHANGAIKO YA SHA SIKU YA PILI
Wagonjwa katika hospitali za kibinafsi zilizo chini ya muungano wa RUPHA watalazimika kulipia huduma za matibabu kwa pesa taslimu kwa siku ya 2 sasa baada ya hospitali hizo kutangaza kufutilia mbali matumizi ya bima ya afya ya SHA.
Kulingana na muungano huo, serikali ina deni la zaidi ya shilingi bilioni 10 la hospitali hizo ambalo isipolipa, basi wanaotegemea huduma za SHA wataendelea kutaabika.
Katibu wa RUPHA Dakta Brian Lishenga, amesema deni hilo ni malimbikizi ya alichotaja kuwa muda mrefu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































