MAAFISA 8 NAKURU KUHOJIWA NA EACC
Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imewaagiza maafisa 8 wa sasa na wa zamani katika serikali ya kaunti ya Nakuru kufika mbele yake hii leo ili kuhojiwa kuhusu madai ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Miongoni mwa maafisa hao ni mwanasheria wa kaunti hiyo Caleb Nyamwage na afisa mkuu katika wizara ya utumishi wa umma Charles Koech ambao watakuwa wa kwanza kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za ukiukaji wa sheria katika kutoa malipo ya zaidi ya shilingi milioni 20 za huduma za kisheria.
Haya yanajiri siku 3 baada ya gavana wa kaunti hiyo Susan Kihika kupata wakati mgumu kueleza matumizi ya mabilioni ya pesa alipofika mbele ya kamati ya uhasibu katika seneti.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































