#Local News

SHULE 29 ZAFUNGWA GATUNDU KUTOKANA NA MOTO

Shughuli za masomo katika shule 29 za bweni katika eneo la Gatundu South kaunti ya Kiambu zimekwama baada ya shule hizo kufungwa kwa muda usiojulikana kutokana na msururu wa visa vya moto, zikiwa ni wiki chache tangu kuanza kwa muhula wa 3.

Wanafunzi wasiopungua 25 wanaohusishwa na uchomaji wa shule hizo wamekamatwa, washikadau mbali mbali sasa wakishinikiza uchunguzi katika mikasa hiyo ili kuepusha kusambaratishwa kwa masomo.

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa wanafunzi walipanga visa hivyo wakati wa likizo kupitia mitandao ya kijamii, kuhusu malalamishi wanayosema hayajaangaziwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SHULE 29 ZAFUNGWA GATUNDU KUTOKANA NA MOTO

MAAFISA 8 NAKURU KUHOJIWA NA EACC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *