#Local News

G7 YASHUTUMU ‘DHULUMA ZA MAI MAHIU’

Magavana wanawake wakiongozwa na Anne Waiguru wa Kirinyaga, wameshutumu visa vya dhuluma ya kingono dhidi ya watoto wa kike vinavyodaiwa kutekelezwa katika eneo la Mai Mahiu kaunti ya Nakuru.

Kupitia taarifa ya muungano wao wa G7, magavana hao wametaja matukio hayo yaliyomulikwa na shirika la habari la kimataifa BBC, kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu na ukosefu wa utu.

Wameitaka idara ya upelelezi kuanzisha uchunguzi na kuwakamata wahusika.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *