IKULU KITOVU CHA UFISADI- GACHAGUA
Ripoti za ufujaji wa fedha kupitia bima ya afya SHA zimeendelea kuibua mijadala nchini, aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua sasa akidai kuwa bima hiyo ni Sakata ya ufisadi ambayo lengo lake ni kufuja mabilioni ya fedha za mlipa ushuru.
Akizungumza kwenye kaunti ya Kajiado, Gachagua amekariri kauli yake kwa ikulu ndicho kitovu cha ufisadi nchini kupitia kuwahonga wajumbe kutoka maeneo mbali mbali ili kuiunga mkono serikali.
Kauli yake imesisitizwa na viongozi wenza wa upinzani ambao wameapa kuendelea kuiwajibisha serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































