PROFESA MUTUA: POKEENI FIDIA
Mshauri wa rais William Ruto kuhusu masuala ya kikatiba na haki za kibinadamu Profesa Makau Mutua amewaomba wakenya msamaha kwa niaba ya serikali kuhusiana na vifo na majraha yaliyotokea wakati wa maandamano ya vijana kizazi cha Gen Z.
Akizungumza na kituo kimoja cha runinga nchini, Mutua amesikitikia matukio hayo ya mwaka wa 2024 na 2025, akiyataja kuwa yenye uchungu na siyo yaliyokusudiwa kwenye katiba.
Hata hivyo, tayari mwenyekiti huyo wa jopo linaloshughulikia mpango wa fidia
kwa waathiriwa wa maandamano hayo amesisitiza kuwa serikali inajutia
athari za maandamano hayo.
Aidha, Mutua amesema kuwa serikali itahakikisha kuwa haki
inapatikana kwa waliouliwa mbali na kuwawajibisha waliokiuka sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































