KAWU: MGOMO WETU BADO UPO
Muungano wa wafanyakazi wa viwanja vya ndege KAWU umesisitiza kuwa mgomo wao wa kuanzia tarehe 1 mwezi ujao tarehe ungalipo iwapo bodi ya mamlaka ya ndege KAA haitajiuzulu.
KAWU ilitoa notisi ya siku 7, ikisema imekosa Imani na utendakazi wa bodi hiyo kutokana na madai kwamba inatoa nyadhifa za ajira kwa upendeleo au hata kupokea hongo kabla ya kufanya hivyo.
Katibu mkuu wa muungano huo Moss Ndiema anasema mazungumzo na bodi hiyo yamefeli.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































