WALIODHALILISHA BENDERA KUFIKISHWA MAHAKAMANI
Wavulana wawili waliokamatwa na maafisa wa DCI kwa madai ya kuidhalilisha bendera kwa kuikanyaga na kuirusha kiholela wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo.
Muhidin Ahmed mwenye umri wa miaka 14 alikamatwa jana jioni, saa chache baada ya mwenzake Ibrahim Haidar mwenye umri wa miaka 17 kukamatwa.
Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen amesema washukiwa watafunguliwa mashtaka ya kuidhalilisha bendera.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































