#Local News

ODM, UDA ZATOA AMRI KWA KAMATI

Kamati iliyoteuliwa kuangazia utekelezaji wa ajenda 10 zilizo kwenye mkataba wa maelewano kati ya chama tawala cha UDA na ODM imeagizwa kuanza kazi yake mara moja, na kuwasilisha ripoti yake ya mwisho kufikia tarehe 7 mwezi Machi mwaka ujao.

Uamuzi huo uliafikiwa katika mkutano wa pamoja wa wabunge walio wanachama wa vyama hivyo, ulioongozwa na Rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga.

Miongoni mwa majukumu ya kamati hiyo ni ukusanyaji wa maoni utakaopelekewa mazungumzo kati ya wadau kutoka vizazi mbali mbali.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *