OLEKSANDR USYK AWEKA WAZI KICHOCHEO CHAKE
Bingwa wa masumbwi ulimwenguni Oleksandr Usyk amesema anachochewa pakubwa na nidhamu na wala si motisha kuendelea kucheza mchezo huo, baada ya kumbwaga Daniel Dubois katika uwanja wa Wembley jijini London Uingereza kwenye pigano la Jumamosi.
Ufanisi huo wa Jumamosi umemfanya raia huyo wa taifa la Ukraine mwenye umri wa miaka 38 kuwa bingwa dunia kwa wanamasumbwi wa uzani wa juu zaidi yaani Heavyweight kwa mara ya 2
Aidha, ufanisi huo ulikuwa ni mara ya 2 kwake kumbwaga Dubois mwenye umri wa miaka 27, baada ya ufanisi sawa mnamo mwaka 2023 jijini Krakow Poland.
Aliwaambia wanahabari baada ya uhsindi wa Jumamoso kuwa analenga kuendelea na mchezo huo, ila hajafahamu mshindani wake katika pigano lijalo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































