POLISI WATOZWA FAINI KWA KUKOSA KUTOA USHAHIDI
Maafisa 6 wa polisi wametozwa faini ya shilingi 10,000 kila mmoja ama kuhudumia kifungo cha miezi 3 gerezani kwa kukosa kutoa ushahidi wao katika kesi ya mauaji inayomkabili afisa mwingine wa polisi.
Sita hao walikuwa miongoni mwa mashahidi 25 waliotarajiwa kutoa taarifa zao kotini kwenye kesi dhidi ya Ahmed Rashid aliyekuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha pangani na anayedaiwa kuwapiga risasi vijana wawili mwaka wa 2017.
Uamuzi huo umetolewa na jaji wa mahakama ya Kibera Diana Racheal Kavedza.
Imetayarishwa na Maureen Mukhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































