WAKENYA KUPATA UMEME NAFUU KUPITIA MIPANGO YA NISHATI YA JOTOARDHI NA NUKLIA
Serikali kuu ina mpango wa kuweka megawati 53 za ziada za nishati ya mvuke kwenye gridi ya taifa ifikapo mwezi Juni 2026 kwa wastani wa gharama ya Ksh8.9 kwa kilowati-saa, na kuifanya kuwa chanzo cha tatu cha bei nafuu zaidi cha umeme baada ya umeme wa maji na unaogizwa kutoka taifa jirani la Ethiopia.
Uwezo wa ziada utatokana na upanuzi wa mitambo ya Olkaria I na OrPower 22 serikali inaposukuma kupunguza gharama za umeme kwa kaya na biashara kupitia nishati mbadala.
Wakati huo huo, inaripotiwa kuwa serikali inaharakisha mipango ya kuongeza nishati ya nyuklia kwenye gridi ya taifa hatua ambayo inaweza kupunguza zaidi gharama za nishati.
Katibu Mkuu wa Kawi Alex Wachira amefichua kuwa serikali inaelekea katika awamu ya pili ya maendeleo ya nuklia, ikilenga kuwa na nishati ya nuklia kwenye gridi ya taifa ifikapo 2034.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































