UHURU KUONGOZA MKUTANO WA JUBILEE
Rais mstaafu Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuongoza mkutano wa kitaifa wa wajumbe wa chama chake cha Jubilee, mkutano unaotazamiwa kutoa mwelekeo wa chama hicho kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Duru zimearifu kuwa Kenyatta ameitisha mkutano huo katika maandalizi ya uchaguzi huo, ikiwemo kumtangaza aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiang’i kama mgombeaji wa urais kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Jeremiah Kioni ni katibu mkuu wa Jubilee.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































