#Sports

KIKOSI CHA BASEBALL CHAINGIA HATUA YA ROBO FAINALI

Kikosi chaka kenya kwenye Kombe la Dunia la Baseball5,kilishangaza wengi baada ya  kukiuka matarajio ya wengi na  kupata nafasi ya kutinga robo fainali mjini Mexico.

Katika mchuano huo unaotawaliwa na wacheza uzani mzito duniani, chipukizi wa Kenya wameibuka kuwa timu iliyoibuka kidedea ya mashindano hayo.

Safari yao kutoka chini hadi kwa washindani wakubwa imeteka hisia za kimataifa na kuibua fahari ya kitaifa kurejea nyumbani.

Baada ya kuanza kwa mshangao dhidi ya timu iliyoorodheshwa sana ya Uropa, Kenya ilishuka kwa seti ya kwanza lakini ikarejea kwa kunguruma ya pili kwa ushindi mkubwa wa 7-1.

Muonekano huu pekee ulikuwa hatua ya ujasiri, lakini maonyesho yao yameonyesha kuwa wako hapa sio tu kushiriki, lakini kushinda.

Huku mpinzani wao mwingine bado hajajulikana kwenye robo fainali , Kocha Wangicho bado yuko na matumaini makubwa katika michezo hii inayoendelea.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KIKOSI CHA BASEBALL CHAINGIA HATUA YA ROBO FAINALI

MSHTUKO KERICHO, JAMAA AWAUA WATU 3

KIKOSI CHA BASEBALL CHAINGIA HATUA YA ROBO FAINALI

KENYA YASHINDA MEDALI KATIKA MBIO ZA DUNIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *