#Sports

UGANDA YATANGAZA BEI NAFUU YA TIKETI YA CHAN

Huku zikiwa zimesalia siku 17 tu kabla ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN), Uganda imetangaza bei nafuu za tiketi ikilinganishwa na waandaji wenza Kenya.
Uganda imeweka tiketi za kawaida USD1 (takriban Ksh129 na UGX3,586) huku tikiti za VIP zikiuzwa kwa USD2 (takriban Ksh258 na UGX7,052).
Itagharimu mashabiki USD3 pekee (takriban Ksh387 na UGX10,578) kupata tiketi ya VVIP.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa LOC ya Uganda Dennis Mugimba, bei hiyo ni matokeo ya ushauri wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuhakikisha tiketi zinauzwa kwa bei nafuu hasa kwa wenyeji.
Nchini Kenya, tiketi za kawaida zitauzwa kwa Ksh200 huku VIP na VVIP zikiuzwa kwa Ksh500 na Ksh1,000 mtawalia.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya ya raga ya wachezaji 15 Samuel Ovwamu ameelezea kusikitishwa kwake na kushindwa kwa timu hiyo kufuzu kwa Kombe la Dunia la Raga 2027 baada ya kushindwa na Zimbabwe.
Ovwamu, ambaye anachezea Menengai Oilers katika ligi kuu nchini amekiri kuwa morali iko chini wakiwa kambini kabla ya mechi yao ya mwisho dhidi ya Algeria.
Ovwamu ambaye alikuwa na msimu mzuri wa kwanza katika ligi kuu nchini hajaanzishwa kwenye mechi yoyote ya Simbas nchini Uganda na anatumai kupata nafasi mechi ya mwisho tarehe 19 Julai 2025.
Kenya walikuwa na matumaini ya kucheza mechi yao ya kwanza katika Kombe la Dunia la Raga lakini ndoto hiyo italazimika kusubiri hadi 2031.

Imetayarishwa na Nelson Andati

UGANDA YATANGAZA BEI NAFUU YA TIKETI YA CHAN

SHIKANGWA AONDOKA SIMA QUEENS 

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *