PENGO LA MALIPO YA CHAI YA KTDA LAZUA GHASIA MIONGONI MWA WAKULIMA
Tofauti kubwa katika malipo ya bonasi ya chai na viwanda 77 vinavyosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Chai nchini (KTDA) imewakera wakulima, huku wengi wao wakirekodi mapato ya chini kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2025. Ripoti ya muda inaonyesha kuwa wakulima katika maeneo bunge 21 yanayolima chai walishuhudia kushuka kwa bei ya majani kwa kati ya senti 0.80 na shilingi 19.10, kwa kilo moja ya majani na kusababisha wakulima wadogo wadogo 680,000 kuathirika na hali hiyo ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Kulingana na ripoti, Wakulima katika eneo la Mashariki mwa bonde la Ufa watapokea kati ya shilingi 26 na shilingi 57 kwa kila kilo katika malipo ya pili, huku wale wa Magharibi mwa bonde la ufa wakipata shilingi 10 hadi shilingi 32 pekee kwa kilo. Hata hivyo, Kiwanda cha Chai cha Kiru kimerekodi anguko kubwa zaidi, kikishuka hadi shilingi 32 kutoka shilingi 51.10 mwaka jana, huku Kiwanda cha Chai cha Rukuriri kikiongoza kwa shilingi 57.50 licha ya kupungua kutoka shilingi 61.50.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































