#Local News

NPS: TUTAHAKIKISHA MAKURUTU WANASAJILIWA

Idara ya polisi imewahakikishia vijana waliokuwa wakilenga kujiunga na vikosi vya polisi kwamba inatafuta njia nyingine za kisheria ili kuendesha zoezi la usajili wa makurutu lililosimamishwa na mahakama kuu hapo jana.

Kupitia taarifa, msemaji wa polisi Muchiri Nyaga amesema idara hiyo itaendelea kuheshimu wa mahakama, huku ikisaka njia mbadala kuhakikisha kuwa vijana 10,000 wanajiunga na idara hiyo haraka iwezekanavyo.

Kesi ya kusimamishwa kwa zoezi hilo iliwasilishwa na mbunge wa zamani Haron Mwau, akitaka mwaznzo mzozo kati ya idara ya polisi NPS na tume ya huduma za polisi NPSC kuhusu usimamizi wa rekodi za malipo yaani payroll utatuliwe.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

NPS: TUTAHAKIKISHA MAKURUTU WANASAJILIWA

FAMILIA KILIFI YALILIA HAKI KWA MWANAO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *