RIPOTI YAFICHUA SHULE HEWA
Zaidi ya shule hewa 20 zimekuwa zikipokea mamilioni ya pesa katika kipindi cha miaka 4 iliyopita, mkaguzi wa hesabu za serikali Nancy Gathungu akiibua hofu kuhusu uwezekano wa wizara ya elimu kutumia mbinu hizo kufuja fedha za wakenya.
Kwenye ripoti ya uchunguzi ulioendeshwa katika shule 400 nchini, mkaguzi huyo aidha amebaini kuwa shule hizo hazimo katika sajili ya wakurugenzi wa elimu wa kaunti, licha ya uwepo wa akaunti za benki ambazo zimekuwa zikipokea fedha.
Aidha, amebaini kuwa shule zinakumbana na changamoto za kifedha, hatua ambayo huenda ikawalazimu wakuu wa shule kufunga shule mapema.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































