#Local News

EACC YAMNASA CHIFU KAKAMEGA

Tume ya maandili na kukabili ufisadi EACC imemkamata chifu wa kata ya Marama Central kaunti ya Kakamega Patrick Oyalo kwa madai ya kuitisha hongo ya shilingi elfu 10 kutoka kwa familia moja ili ipate hatimiliki ya shamba baada ya kifo cha baba wa familia hiyo.

Hatua hiyo imejiri chini ya siku moja baada ya EACC kuwasilisha ripoti kuhusu kiwango cha ufisadi nchini, ikiorodhesha afisi za machifu kama baadhi ya maeneo ambako uovu huo umeenea.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *