KEPSA YASHINIKIZA USHIRIKIANO MPYA AGOA
Muungano wa Sekta ya Kibinafsi nchini Kenya (KEPSA) umeitaka Marekani kutayarisha upya Sheria ya Ukuaji na Fursa Afrika (AGOA) kwa kipindi cha miaka 16, ikionya kuwa kushindwa kufanya hivyo kunaweza kuyumbisha kazi na mtiririko wa uwekezaji katika nchi zote mbili.
Akizungumza katika Jukwaa la Uwekezaji mjini New York, Mkurugenzi Mtendaji wa KEPSA Carole Kariuki amesema kwamba iwapo ushirikiano wa kiabiashara hautaendelea, Washington inapaswa kuipa Kenya kipindi cha mpito cha miaka miwili ili kujadili mkataba wa biashara baina ya nchi hizo mbili.
Kenya iliuza nguo za thamani ya dola milioni 470 kwa Marekani mwaka wa 2024, kutoa fursa za kazi za moja kwa moja 66,800, robo tatu yao wakiwa wanawake. KEPSA inakadiria kuwa karibu maisha ya watu 800,000 yanategemea mauzo ya nje yanayohusiana na AGOA.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































