WAKENYA WAMWOMBOLEZA MBUNGE WA ZAMANI
Viongozi na wakenya kutoka matabaka mbali mbali wameendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa mbunge wa Rongo na Waziri Dalmas Otieno aliyefariki hapo jana akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kupitia ujumbe, Rais William Ruto amemwomboleza Otieno kama kiongozi mwenye maono aliyelitumikia taifa kwa maadili, huku kinara wa ODM Raila Odinga akimtaja mwendazake kama mtumishi wa umma aliyeamini utumishi bora wa umma kama msingi wa uongozi bora.
Otieno alichaguliwa kwa mara kwanza kama mbunge mwaka wa 1988, na pia akahudumu kama Waziri katika serikali ya marais wastaafu Daniel Moi na Mwai Kibaki.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































