#Local News

KURIA AKOSOA VITISHO VYA DUALE DHIDI YA MISHRA

Aliyekuwa mshauri mkuu wa rais William Ruto kuhusu masuala ya uchumi Moses Kuria, amekosoa vitisho vya waziri wa Afya Aden Duale vya kumpokonya uraia aliyekuwa mbunge wa Kesses kaunti ya Uasin Gishu Swarup Mishra kuhusiana na madai kwamba hospitali ya Mishra inajihusisha na ulanguzi wa viungo vya mwili wa binadamu.

Kupitia taarifa, Kuria amesema tangazo la kiholela kama hilo linawatishia wawekezaji wa kigeni kuwekeza humu nchini, akishindwa nia vipi Duale akatoa tangazo hilo ilhali hahudumu katika idara ya uhamiaji.

Aidha, amesema kauli hiyo itaathiri mpango wa serikali wa kuwapa ajira vijana kwa kuwatishia wawekezaji.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KURIA AKOSOA VITISHO VYA DUALE DHIDI YA MISHRA

KESI DHIDI YA GAKUYA KUREJELEWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *