MOFA YAIMARISHA MAJARIBIO YA WACHEZAJI KUJIUNGA NA KILABU HIYO
Majaribio ya wachezaji kujiunga na kituo cha soka cha Michael Olunga Foundation Academies U16 yanazidi kushika kasi, huku Mkurugenzi wa Kiufundi wa MOFA Aol Omondi akithibitisha tena dhamira ya programu hiyo ya kuibua na kukuza vipaji vya soka kote nchini Kenya.
Akizungumza baada ya mkondo wa majaribio Kisumu, Omondi alisisitiza umuhimu wa kusonga mbele zaidi ya mashindano ya shule ili kufikia wachezaji wengi wachanga.
Omondi aliongeza kuwa mpango wa muda mrefu wa taasisi hiyo ni kuandaa wachezaji katika viwango vya kimataifa huku wakisaidia elimu, kipengele muhimu cha mpango mkakati wa MOFA wa 2026-2028, ambapo kupanda hadi ligi kuu inasalia kuwa lengo kuu.
Majaribio hayo sasa yatahamia mikoa mingine, jana walikuwa Migori, leo wako Bungoma, Malindi na Homa Bay ni tarehe 21, Mombasa tarehe 22, Kilifi tarehe 23, na Kakamega tarehe 24 mwezi huu.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































