#Local News

UPINZANI WADAI NJAMA YA KUSAMBARATISHWA

Mrengo wa upinzani umeibua madai kwamba kuna njama ya kuusambaratisha mrengo huo kwa kuwashawishi baadhi ya viongozi wake wajiunge na serikali ili kumhakikishia Rais William Ruto muhula wa pili madarakani.

Wakizungumza katika eneo la Isinya kaunti ya Kajiado, viongozi hao wakiongozwa na aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua, wameshikilia kuwa jududi hizo hazitafaulu, na kwamba watafanya kikao ili kumteua mmoja wao kumenyana na Rais Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Viongozi wengine waliokuwa wameandamana na Gachagua ni kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, na mwenzake wa DAP-K Eugene Wamalwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UPINZANI WADAI NJAMA YA KUSAMBARATISHWA

ODM: HATUTAKUWA TENA UPINZANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *