MAKOMREDI KUANZA MGOMO LEO
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma wameratibiwa kujiunga na wahadhiri wao kwenye mgomo wa kitaifa hii leo kwa lengo la kuishinikiza serikali kutatua mgomo wa wahadhiri ili kufanikisha kurejelea shughuli za masomo.
Viongozi wa wanafunzi hao wamesema wanahofia huenda mgomo huo ukaathiri kalenda ya masomo yao iwapo hautatuliwa mapema, huku wahadhiri wakishikilia kuwa hawatarejea kazini hadi mkataba wa maelewano wa mwaka wa 2017-21 utakapotekelezwa
Huku hayo yakijiri, Waziri wa elimu Julius Ogamba amewaambia maseneta kuwa wizara yake haijaelewa kiwango kamili cha fedha wanazodai wahadhiri.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































