WAGONJWA WALIOPONA WAZUILIWA MTRH
Akina mama 27 waliojifungua maajuzi wameendelea kuzuiliwa katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi jijini Eldoret baada ya kushindwa kulipa ada za matibabu.
Kwenye kanda ya video iliyosagaa kwenye mitandao ya kijamii, akina mama hao, baadhi wakidai kuzuiliwa kwa zaidi ya miezi 3 licha ya kuwa katika hali nzuri, wameibua madai ya kupitishiwa katika hali ngumu na usimamizi wa hospitali hiyo.
Hata hivyo, usimamizi wa hospitali hiyo umekana madai ya kuwahangaisha, ukisema waliozuiliwa ni akina mama wasio na vyeti vya utambulisho kutokana na umri wao mdogo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































