MASOMO YA WANAFUNZI NJIA PANDA
Hatma ya masomo ya wanafunzi katika shule za msingi na upili sasa iko kwenye njia panda, kufuatia tangazo la serikali kwamba haiwezi kufadhili kikamilifu elimu ya bure katika shule za msingi na upili za umma kutokana na uhaba wa fedha.
Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya elimu katika bunge la kitaifa, waziri wa fedha John Mbadi, amesema kati ya shilingi elfu 22 kwa kila mwanafunzi wa shule ya upili, serikali itamudu shilingi elfu 16,900 pekee.
Nao wabunge wamekosoa mfumo wa sasa wa kuwasajili wanafunzi KEMIS, wakisema umewaacha nje wengi wa wanafunzi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































