GACHAGUA ATANGAZA AZMA YA URAIS
Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua hatimaye ameweka wazi kwamba atawania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, akiahidi kudhibiti deni linalolikabili taifa mbali na kuimarisha uchumi wa nchi iwapo atachaguliwa.
Kulingana na kiongozi huyo wa chama cha DCP, atafuata nyayo za rais mstaafu marehemu Mwai Kibaki, mbali na kufutilia mbali baadhi ya sera zilizowekwa na rais William Ruto.
Miongoni mwa sera hizo ni kupunguza ushuru unaotozwa wafayakazi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































