#Local News

SERIKALI YAGEUKIA WAKOPESHAJI WAPYA KUJAZA PENGO LA ADANI

Serikali kuu imeanza mikakati ya kutafuta mkopeshaji mwingine baada ya ushirikiano wake na kampuni ya Adani wa kufadhili upanuzi uliopangwa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kufeli.

Kulingana na waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir, serikali tayari imeandika barua kwa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA), Benki ya Exim ya China, Benki ya Maendeleo ya KFW (kampuni ya Ujerumani), Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (FIB), na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Hata hivyo shughuli ya kupanua uwanja wa ndege wa kimataifa ilikwama baada ya serikali kufuta mpango huo wenye utata wa Adani. Mpango huo ulisitishwa baada ya shinikizo la umma kufuatia kufunguliwa mashtaka kwa maafisa wa kampuni hiyo ya India kwa hongo na ulaghai. Serikali inatafuta kuchangisha shilingi bilioni 258 ili kufanikisha mradi huo.

Imetayarishwa na Maureen Amwai

SERIKALI YAGEUKIA WAKOPESHAJI WAPYA KUJAZA PENGO LA ADANI

GACHAGUA AKATIZA ZIARA MAREKANI

SERIKALI YAGEUKIA WAKOPESHAJI WAPYA KUJAZA PENGO LA ADANI

MAHAKAMA YAMJIBU RAIS RUTO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *