#Local News

WAKENYA MILIONI 2.2 KUTIBIWA BURE, RAIS

Wakenya milioni 2.2 walio na mapato ya chini wamepata afueni ya matibabu baada ya serikali kutangaza kuwa itakuwa ikiwalipia ada za SHA ili kugharamia matibabu yao.

Tangazo hilo limetolewa na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi, akisema mpango huo utawawezesha walengwa kupokea huduma za matibabu bila malipo katika hospitali za humu nchini.

Kulingana na rais, mpango huo ni sehemu ya serikali kuimarisha mpango wa huduma za afya kwa wote UHC.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *