#Local News

MWANGA WA USALAMA KERIO

Walimu katika bonde la Kerio wamepongeza operesheni  ya usalama
inayoendelea  katika maeneo hayo  wakisema kuwa hatua hiyo
imerejesha  imani  miongoni mwa wanafunzi na  kufufua mahudhurio
shuleni.

Katibu wa muungano wa walimu KNUT, tawi la Elgeyo Marakwet John
Chebari amesema kuwa zaidi ya shule 35 ambazo zilikuwa zimefungwa au
kuathirika kwa visa vya uhalifu zinatarajiwa kurejelea shughuli za kawaida.

Hata hivyo, Chebari ameitaka serikali kudumisha hatua za sasa za
usalama ili  wanafunzi wafurahie masomo kama wenzao na shughuli za
kawaida pia zirejelewe katika maeneo hayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MWANGA WA USALAMA KERIO

EKITIKE AOMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI

MWANGA WA USALAMA KERIO

MAZUNGUMZO YA MIKOPO YA IMF YAANZA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *