#Local News

KESI DHIDI YA GAKUYA KUREJELEWA

Kesi ya ufisadi inayohusu madai ya ufujaji wa shilingi milioni 40 inayomkabili mbunge wa Embakasi North James Gakuya inarejelewa hii leo katika mahakama inayosikiliza kesi zinazohusiana na ufisadi jijini Nairobi.

Gakuya aanakabiliwa na mashtaka manne ikiwemo mgongano wa maslahi kwa madai kwamba alitoa kandarasi za ujenzi wa barabara kwa kampuni zilizo na uhusiano wa karibu naye.

Mashtaka mengine ni njama ya ulaghai, ukiukaji wa sheeria za ununuzi na uporaji wa mali ya umma.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *