FKF KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUBADILISHA SEKTA YA MICHEZO
Wizara ya Michezo imethibitisha kujitolea kwake kufanya kazi bega kwa bega na mashirikisho yote ya michezo kote nchini ili kubadilisha sekta ya michezo ya Kenya kupitia ukuzaji wa miundombinu, utawala dhabiti na mageuzi ya kitaasisi.
Akizungumza baada ya kikao cha mashauriano na uongozi wa zaidi ya mashirikisho na vyama 140 vya michezo huko Kasarani Jumatano, Waziri wa Michezo Salim Mvurya alisisitiza kwamba kuwekeza katika miundomsingi ya kisasa kote nchini ni muhimu katika kuibua vipaji vya mashinani na kuiweka Kenya kama kitovu cha michezo duniani.
Alibainisha kuwa wakati Mfuko wa Michezo upo, si hundi tupu bali unafanya kazi kwa kufuata miongozo madhubuti ya Serikali na mzunguko wa fedha wa kila mwaka hivyo kuyataka mashirikisho kuboresha mifumo yao ya kiutawala kama sehemu ya kuvutia uwekezaji wa kutosha kutoka sekta binafsi.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































