#Sports

AKONNOR KUTUMIA MCHEZO WA SIMBA KUREKEBISHA KIKOSI

Kocha mkuu wa Gor Mahia Charles Akonnor anasema mechi ya Simba iliwapa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya FKF picha kamili ya walipo na nini cha kurekebisha kuelekea msimu mpya.

Mchezo huo uliochezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuadhimisha siku ya Simba Day, ulishuhudia K’Ogalo wakiwachabangwa 2-0 kupitia kw amabao ya wachezaji Mohammed Hamza na Steven Mukwala waliofunga wababe hao wa Tanzania.

Mohammed alifunga bao la kuongoza dakika ya sita kwa kichwa kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Saleh kabla ya Mukwala kupachika bao la pili mapema kipindi cha pili baada ya Sylvester Owino kushindwa kuamsha krosi hatari ndani ya eneo la sita.

Raia huyo wa Ghana aliwasifu vijana wake licha ya kupoteza, akibainisha kuwa mabao yake yalikuja kama matokeo ya mchezo huo.

Imetayarishwa na Nelson Andati

AKONNOR KUTUMIA MCHEZO WA SIMBA KUREKEBISHA KIKOSI

FAINALI YA DALA SEVENS

AKONNOR KUTUMIA MCHEZO WA SIMBA KUREKEBISHA KIKOSI

DABI YA MANCHESTER

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *