RAIS BIYA AFANYIA MAGEUZI UONGOZI WA JESHI
Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 92, ambaye ni kiongozi wa taifa mkongwe zaidi ulimwenguni kwa sasa amefanya mageuzi katika safu za juu za jeshi lake, wachanganuzi wakisema hatua hiyo inalenga kumhakikishia ushindi kwenye uchaguzi wa urais mwezi Oktoba mwaka huu.
Mageuzi hayo yamefanywa katika vitengo vyote vya jeshi, ikiwemo uteuzi wa msimamizi wa wafanyakazi wa jeshi la nchi kavu, angani na majini mbali na kuwapandisha madaraka mabrigadia jenerali 8 hadi ngazi ya meja jenerali.
Mageuzi hayo yamejiri siku 2 baada Biya ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka wa 1982, kutangaza kuwa atatea kiti chake kwenye uchaguzi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































