WANARIADHA 50 KUELEKEA TOKYO JAPAN
Mwenyekiti wa Riadha Kenya tawi la Nairobi Barnaba Korir anasema wanapanga kupeleka wanariadha zaidi ya 50 kwenye Mashindano yajayo ya Riadha ya Dunia yanayopangwa Tokyo Japan.
Akizungumza kabla ya Majaribio ya Kitaifa, yanayotarajiwa kuanza Jumanne katika Uwanja wa Ulinzi Sports Complex, Korir alisema idadi hiyo inaweza kuongezeka ikiwa wanariadha wengi zaidi watafuzu kwa mashindano hayo. Korir wakati huo huo ameishukuru serikali kwa usaidizi wao.
“Tulikaribia kukosa kuandaa Kip Keino Classic mwaka huu lakini wizara ilipitia na kutusaidia kuandaa shindano hili, na ukiona tata ni kubwa sana kuandaa mashindano ya riadha huko,” alisema. “Tunatumai hata majaribio ya kesho [Jumanne] yatakuwa mazuri kutazama.”
Korir wakati huo huo ametoa changamoto kwa makampuni kujitokeza na kuwatumia wanariadha kama mabalozi wa chapa zao, ili kusaidia kuboresha maisha yao.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































