XHAKA AJIUNGA NA SUNDERLAND
Kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka amejiunga na Sunderland kwa kandarasi ya miaka mitatu, na kurejea Premier League miaka miwili baada ya kuondoka Arsenal na kwenda Bayer Leverkusen.
Xhaka, 32, alikaa Arsenal kwa miaka saba kabla ya kujiunga na Leverkusen, ambapo alishinda Bundesliga na kufika fainali ya Ligi ya Europa katika msimu wake wa kwanza.
Hakuna ada iliyofichuliwa kwa uhamisho huo lakini ripoti za vyombo vya habari vya Uingereza zilisema Sunderland ilimsajili Xhaka kwa pauni milioni 17.3 ($23.14 milioni).
Hatua ya kujiunga na klabu hiyo mpya iliyopanda daraja ya Ligi ya Premia inakuja wiki moja baada ya meneja wa Leverkusen Erik ten Hag kusema Xhaka alikuwa muhimu sana kwa klabu hiyo kumwachilia.
Xhaka, ambaye ameichezea Arsenal mechi 225 za Ligi Kuu ya Uingereza, alishinda Kombe la FA mara mbili akiwa na timu hiyo ya Kaskazini mwa London.
Sunderland wanaanza kampeni zao za ligi kwa mechi ya nyumbani dhidi ya West Ham United mnamo Agosti 16.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































