#Sports

KCB RFC WATAWAZWA MABINGWA WA DALA 7S, NATIONAL CIRCUIT

Klabu na raga ra KCB RFC ndio mabingwa wa kipute cha 2025 Dala 7s baada ya kustahimili ushindani kutoka kwa mahasimu wao Kabras RFC kwa ushindi wa 12-7 katika fainali za mashindano hayo kwenye uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Kisumu.

Kabla ya ubingwa huo, wanabenki hao tayari walikuwa wametawazwa mabingwa wa jumla wa mashindano ya National 7s Circuit  mapema baada ya ushindi wa 15-14 katika robo fainali za dala 7s dhidi ya Strathmore Leos, ambao ni washindani wao wa karibu.

Huku hayo yakijiri, Daystar falcolns waliwacharaza Menengai oilers 31:0 na kujipatia nafasi ya 3, nao Nakuru RFC wakawapiku Mwamba RFC 17-10 katika fainali za kusaka nafasi ya 5

Wakati uo huo, Catholic Monks waliwacharza Impala RFC 26-7 na kutawazwa mabingwa wa Challenger Cup, huku Masinde Muliro University wakiwazidi Kisumu kwa 31-0 katika kuwania nafasi ya 13.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *