KWAHERI OTP, INGIA DIJITALI
Shughuli za matibabu chini ya bima ya afya ya serikali SHA zinatarajiwa kurahishwa baada ya serikali kuondoa mfumo wa uthibitisho wa OTP, uliowataka wakenya kusubiri ujumbe kwenye simu zao kabla ya kuhudumiwa.
Akitangaza kusitishwa rasmi kwa mfumo huo, waziri wa afya Aden Duale amesema watumiaji wa bima hiyo watahitajika kujisajili upya kupitia mfumo wa kiidijitali.
Hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa matibabu kupitia SHA mbali na kupunguza ulaghai uliiokuwa ukiendelezwa na baadhi ya hospitali nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































