SHULE KULAZIMIKA KUFUNGA MAPEMA
Masomo katika shule za umma nchini yatalazimika kukatizwa mapema muhula huu kutoka na uhaba wa fedha, wakuu wa shule hizo wakisema hawana uwezo wa kuziendesha shule baada ya serikali kukosa kutuma mgao wa masomo.
Changamoto za kifedha shuleni zimesababishwa na mgao kupunguzwa, kucheleweshwa au hata kutotumwa kwa shule ili kufanikisha shughuli za kila siku.
Katika kikao na wanahabari, muungano wa KUPPET umeonya kuwa huenda wazazi wakalazimika kulipa karo ya ziada muhula ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































