#uncategorized

MAFUTA YAPUNGUA KWA SHILINGI 1

Bei ya mafuta ya petroli imepungua kwa shilingi moja kila lita huku ile ya diseli na mafuta taa ikisalia jinsi ilivyokuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Hii baada ya mamlaka ya kudhibiti kawi EPRA kutoa bei mpya za bidhaa hiyo kwa kipindi cha kati ya tarehe 15 mwezi huu hadi tarehe 14 mwezi ujao, ikisema bei ya uagizaji wa mafuta kutoka nje ilipungua kwa kiasi kidogo.

Lita ya petroli jijini Nairobi sasa itauzwa kwa shilingi 185.31, nayo diseli na mafuta taa ikisalia shilingi 171.58 na 155.58 mtawalia.

Imetayarishwa na Maureen Amwai

MAFUTA YAPUNGUA KWA SHILINGI 1

MAHAKAMA KUAMUA UUGIZAJI WA MCHELE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *