#Local News

KESI YA MVUVI BRIAN YAAHIRISHWA

Kesi inayohusiana na mvuvi aliyetoweka katika eneo la Nakuru Brian Odhiambo itaendelea tarehe 1 mwezi Septemba baada ya kikao cha kusikilizwa kwa kesi hiyo kuahirishwa hapo jana.

Wakati wa kikao hicho, mtaalamu wa deta za mawasiliano, Hassan Salado, alifichua kuwa simu ya Odhiambo ilionekana mara ya mwisho eneo sawa na zile za maafisa 4 wa idara ya KWS ambao ndio washukiwa wakuu katika tukio la kutoweka kwa mvuvi huyo mnamo tarehe 18 mwezi Januari mwaka huu.

Wanne hao ni Alexander Lorogoi, Isaac Odhiambo, Michael Wabukala, na Evans Kipsang, ambao mahakama ilifahamishwa kwamba wangali kazini licha ya kukabiliwa na kesi ya uhalifu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KESI YA MVUVI BRIAN YAAHIRISHWA

KESI YA REX KUENDELEA LEO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *