#Local News

USALAMA KWENYE FOLENI

Ni afueni kwa wakazi wanaoishi kwenye mpaka wa Kenya na Somalia baada ya wanajeshi kuweka kambi yao eneo hilo itakayoaimarisha doria na kuwahakikishia wakazi wa eneo hilo linaloongozwa na Kenya Leaders Engagement usalama wao.

Muungano huo umeleta pamoja vyombo vya usalama, wasimamizi na
wakazi katika eneo hilo ambalo limekumbwa mashambulizi ya mara kwa mara wa magenge ambayo huwalenga wanajeshi.

Meja Martin Kasinga amesema kuwa zoezi la kulinda eneo hilo
linastahili ushirikiano kutoka pande zote, lengo kuu la kikosi
hicho likiwa ni kuleta amani  na utulivu  katika mpaka wa Kenya na
Somalia.


Wakazi wakiongozwa na Omar Hussein wamekaribisha mpango huo wakiwapongeza wanajeshi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kuwa  eneo hilo linasalia kuwa tulivu.

Aidha, wameahidi kushirikiana na jeshi ili kuhakiikisha magenge ya uhalifu yanakomeshwa ili kufanikisha ukuaji wao wa kiuchumi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

USALAMA KWENYE FOLENI

JIANDAENI KWA MEZA KAVU, WAKENYA WAONYWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *