KENYA YAPTA HOLIDEI MPYA
Rais William Ruto amechapisha rasmi tarehe 27 mwezi Agosti kuwa siku ya kusherehekea katiba yaani Katiba Day, hafla itakayokuwa ikiadhimishwa kila mwaka kuadhimisha kupitishwa kwa katiba ya mwaka 2010.
Kupitia tangazo hii leo, Ruto amesema siku hiyo itakuwa ikiadhimishwa ili kuwakumbusha wakenya kuhusu wajibu wao wa kuidumisha, kulinda na kutekeleza katiba hiyo.
Maadhimisho ya kwanza ya sherehe hiyo yatafanyika tarehe 27 mwezi huu ambayo Jumatano wiki hii.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































