14 WAKAMATWA KITALE
Maafisa wa polisi kutoka vitengo mbali mbali wamewakamata washukiwa 14 wa msururu wa visa vya uhalifu mjni Kitale.
Kulingana na idara ya upelelezi wa jinai DCI, washukiwa wamekamatwa katika maeneo ya Umoja, Kisumu Ndogo, Tuwan, Bondeni na Mitume kufuatia operesheni iliyoratibiwa vyema.
Aidha, imesema inawahoji washukiwa kabla ya kuwafikisha mahakamani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































